قَالَ لَهُۥ صَاحِبُهُۥ وَهُوَ يُحَاوِرُهُۥٓ أَكَفَرۡتَ بِٱلَّذِي خَلَقَكَ مِن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ سَوَّىٰكَ رَجُلٗا ٣٧
Qāla lahū sāhibuhū wahuwa yuhāwiruhū akafarta billadhī khalaqaka min turābin thumma min nutfatin thumma sawwāka rajulā
Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je! Unamkufuru aliye kuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mtu kaamili? 37
Maelezo ya chini
37 Mwenzie Muumini akamjibu: Unajiachilia kumkufuru Mola wako Mlezi aliye kuumba tangu asli yako ya Adam kutokana na udongo, kisha kutokana na tone ya maji-maji ya mbegu ya uzazi, kisha akakufanya mtu aliye kamilika? Ikiwa unajiona bora kwa mali yako na jamaa zako, basi mkumbuke Mola wako Mlezi na asli yako ya udongo.