Surat Al-Kahf, aya 32

18:32

۞ وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلٗا رَّجُلَيۡنِ جَعَلۡنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيۡنِ مِنۡ أَعۡنَٰبٖ وَحَفَفۡنَٰهُمَا بِنَخۡلٖ وَجَعَلۡنَا بَيۡنَهُمَا زَرۡعٗا ٣٢

Wadrib lahum mathalar rajulayni ja'alnā li ahadihimā jannatayni min a'nābin wahafafnāhumā binakhlin waja'alnā baynahumā zar'ā

Na wapigie mfano wa watu wawili: mmoja wao tulimpa vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende, na kati yake tukatia mimea ya nafaka. 32

Maelezo ya chini

32 Ewe Mtume! Bainisha baina ya hali ya makafiri matajiri na Waumini mafakiri kwa kuwapigia mfano ulio tokea hapo zamani baina ya watu wawili: kafiri na Muumini. Huyo kafiri alikuwa na vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende kwa ajili ya pambo na faida pia. Na baina ya hivyo vitalu tukaweka makulima mengine yaliyo stawi na kutoa mazao.