وَٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِهِۦ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلۡتَحَدٗا ٢٧
Watlu mā ūhiya ilayka min kitābi rabbika lā mubaddila likalimātihī walan tajida min dūnihī multahadā
Na soma uliyo funuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hapana wa kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio isipo kuwa kwake. 27
Maelezo ya chini
27 Ewe Mtume! Soma uliyo funuliwa kwa wahyi katika Qur'ani. Na katika hayo yamo uliyo funuliwa ya khabari za hao vijana. Wala usisikilize hayo maskhara yao ya kutaka ubadilishe muujiza wa Qur'ani kwa muujiza mwingine. Kwani hakika hapana wa kuyageuza anayo simulia Mwenyezi Mungu maneno ya haki katika miujiza yake. Hakika hapana awezae kubadilisha hayo. Wala usende kinyume na amri ya Mola wako Mlezi, kwani hapo tena hutapata wa kumkimbilia kukuhifadhi naye.