ثُمَّ جَعَلۡنَٰكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡرِ فَٱتَّبِعۡهَا وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ ١٨
Thumma ja'alnāka 'alā sharī'atim minal-amri fattabi'hā walā tattabi' ahwā'al-ladhīna lā ya'lamūn
Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu. 18
Maelezo ya chini
18 Tena tukakujaalia wewe, ewe Muhammad, baada ya khitilafu za Watu wa Kitabu (yaani Mayahudi na Wakristo), kuwa ni Mtume wa kwenda Njia iliyo wazi katika mambo ya Dini tuliyo kuwekea wewe na walio kuwa kabla yako miongoni mwa Mitume. Basi ifuate Sharia yako ya Haki, yenye kuthibiti imara kwa hoja na dalili, wala usifuate matamanio ya watu wasio ijua Njia ya Haki.