أَوۡ يَكُونَ لَكَ بَيۡتٞ مِّن زُخۡرُفٍ أَوۡ تَرۡقَىٰ فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَن نُّؤۡمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيۡنَا كِتَٰبٗا نَّقۡرَؤُهُۥۗ قُلۡ سُبۡحَانَ رَبِّي هَلۡ كُنتُ إِلَّا بَشَرٗا رَّسُولٗا ٩٣
Aw yakūna laka baytum min zukhrufin aw tarqā fis-samā'i walan nu'mina liruqiyyika hattā tunazzila 'alaynā kitāban naqra'uhū qul subhāna rabbī hal kuntu illā basharar rasūlā
Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na Mtume? 93
Maelezo ya chini
93 Au uwe na nyumba iliyo pambwa kwa dhahabu, au upae mbinguni. Na hata hivyo hatukusadiki mpaka ukituletea kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha ukweli wako tukisome! Waambie: Mola wangu Mlezi ametakasika kabisa na kuhukumiwa na yeyote, au yeyote kushirikiana naye katika kudra yake! Mimi si chochote ila ni mwanaadamu kama Mitume wote wengineo. Na wala wao hawakuwaletea watu wao muujiza ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.