Surat Al-Isra, aya 80

17:80

وَقُل رَّبِّ أَدۡخِلۡنِي مُدۡخَلَ صِدۡقٖ وَأَخۡرِجۡنِي مُخۡرَجَ صِدۡقٖ وَٱجۡعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلۡطَٰنٗا نَّصِيرٗا ٨٠

Waqur rabbi adkhilnī mudkhala sidqin wa akhrijnī mukhraja sidqin waj'al lī mil ladunka sultānan nasīrā

Na sema: Mola wangu Mlezi! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazo toka kwako zinisaidie. 80

Maelezo ya chini

80 Na sema: Ewe Mola Mlezi! Niingize maingizo ya kuridhisha matukufu katika kila unapo niingiza katika jambo au pahala. Na unitoe kwa kutoka kunako ridhisha kutukufu. Na kwa fadhila yako nijaalie nguvu za kunisaidia niwashinde maadui zangu.