Surat Al-Isra, aya 46

17:46

وَجَعَلۡنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ أَكِنَّةً أَن يَفۡقَهُوهُ وَفِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَقۡرٗاۚ وَإِذَا ذَكَرۡتَ رَبَّكَ فِي ٱلۡقُرۡءَانِ وَحۡدَهُۥ وَلَّوۡاْ عَلَىٰٓ أَدۡبَٰرِهِمۡ نُفُورٗا ٤٦

Waja'alnā 'alā qulūbihim akinnatan an yafqahūhu wafī ādhānihim waqran wa idhā dhakarta rabbaka fil-qur'āni wahdahū wallaw 'alā adbārihim nufūrā

Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi. Na unapo mtaja katika Qur'ani Mola wako Mlezi peke yake, basi wao hugeuka nyuma wakenda zao. 46

Maelezo ya chini

46 Na kwa mujibu wa hikima yetu ya kupotoa na kuongoa huweka vifuniko juu ya nyoyo zao, wasipate kuifahamu Qur'ani ilivyo. Na katika masikio yao hutia uziwi basi hawasikii lenye manufaa kwao. Hayo ni kwa sababu ya kupindukia katika inda yao na majivuno yao. Na pale unapo mtaja Mola wako Mlezi katika Qur'ani peke yake bila ya kuwataja miungu yao, wao basi hurejea nyuma wakaacha kukusikiliza.