Surat Al-Isra, aya 26

17:26

وَءَاتِ ذَا ٱلۡقُرۡبَىٰ حَقَّهُۥ وَٱلۡمِسۡكِينَ وَٱبۡنَ ٱلسَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرۡ تَبۡذِيرًا ٢٦

Wa āti dhal-qurbā haqqahū wal-miskīna wabnas-sabīli walā tubaddhir tabdhīrā

Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo. 26

Maelezo ya chini

26 Na wape jamaa zako haki yao kwa kuwafanyia wema na kuwaunga; na kadhaalika masikini mwenye haja, na msafiri aliye katikana na mali yake. Wape hao haki yao katika Zaka na sadaka, wala usiyavuruge mali yako kwa utumiaji ovyo usio na maslaha.