ٱنظُرۡ كَيۡفَ فَضَّلۡنَا بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۚ وَلَلۡأٓخِرَةُ أَكۡبَرُ دَرَجَٰتٖ وَأَكۡبَرُ تَفۡضِيلٗا ٢١
Unzur kayfa faddalnā ba'dahum 'alā ba'din walal'ākhiratu akbaru darajātin wa akbaru tafdīlā
Angalia vipi tulivyo wafadhili baadhi yao kuliko wenginewe. Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi. 21
Maelezo ya chini
21 Hebu angalia kwa kuzingatia vipi tulivyo wafadhilisha baadhi ya waja wetu kuliko wengine, kwa kuwapa mali na vyeo na nafasi, pindi wakishika njia za kuyapata hayo katika dunia. Na hayo ni kwa hikima tunayo ijua Sisi. Na tafauti zao katika Akhera ni kubwa zaidi kuliko tafauti zao za duniani. Kwa hivyo yatakikana waishughulikie Akhera, kwani huko ndiko kwenye kutukuka kwa kweli na kuzidiana kwa hakika.