فَأَرَادَ أَن يَسۡتَفِزَّهُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ فَأَغۡرَقۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ جَمِيعٗا ١٠٣
Fa arāda an yastafizzahum minal-ardi fa aghraqnāhu wamam ma'ahū jamī'ā
Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha yeye na walio kuwa pamoja naye wote. 103
Maelezo ya chini
103 Firauni akashikilia uasi wake, akataka kumtoa Musa na Wana wa Israili katika nchi ya Misri. Tukamzamisha yeye na askari wake wote.