Surat Al-Imran, aya 89

3:89

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ ٨٩

Illal-ladhīna tābū mim ba'di dhālika wa aslahū fa innallāha ghafūrur rahīm

Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. 89

Maelezo ya chini

89 Lakini wale ambao wamejing'oa na madhambi yao, wakaingia kati ya watu wema, wakayaondoa waliyo yaharibu, basi hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atawafutia madhambi yao, kwani maghfira na rehema ni miongoni mwa sifa za dhati yake Tukufu.