وَقَالَت طَّآئِفَةٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ ءَامِنُواْ بِٱلَّذِيٓ أُنزِلَ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَجۡهَ ٱلنَّهَارِ وَٱكۡفُرُوٓاْ ءَاخِرَهُۥ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ ٧٢
Waqālat tā'ifatum min ahlil-kitābi āminū billadhī unzila 'alal-ladhīna āmanū wajhan-nahāri wakfurū ākhirahū la'allahum yarji'ūn
Na kikundi katika Watu wa Kitabu walisema: Yaaminini yale waliyo teremshiwa wenye kuamini mwanzo wa mchana, na yakataeni mwisho wake; huenda wakarejea. 72
Maelezo ya chini
72 Katika mtindo wao wa kutaka kuwapotoa Waumini, hawa Watu wa Kitabu wakiwaambia wenzao: Jitieni kuiamini Qur'ani aliyo teremshiwa Muhammad asubuhi, na ikifika jioni ikataeni. Huenda kwa hivyo mkawafitini hawa kwa kuwaingiza shaka katika nyoyo zao, wakaiacha dini yao.