Surat Al-Imran, aya 47

3:47

قَالَتۡ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٞ وَلَمۡ يَمۡسَسۡنِي بَشَرٞۖ قَالَ كَذَٰلِكِ ٱللَّهُ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ إِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ ٤٧

Qālat rabbi annā yakūnu lī waladun walam yamsasnī basharun qāla kadhālikillāhu yakhluqu mā yashā'u idhā qadā amran fa innamā yaqūlu lahū kun fayakūn

Maryamu akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba apendacho. Anapo hukumu jambo, huliambia: Kuwa! Likawa. 47

Maelezo ya chini

47 Maryamu alisema kwa kustaajabu kupata mwana kwa njia isiyo ya kawaida: Vipi nitapata mwana na ilhali hapana mwanamume aliyenigusa? (yaani aliye lala nami). Mwenyezi Mungu Mtukufu akakumbusha kuwa Yeye huumba atakacho kwa kudra yake bila ya shuruti za sababu zilizo zowewa. Kwani Yeye akitaka jambo hulileta tu kwa taathira ya uwezo wake katika atakalo bila ya kutafuta kinginecho cha kutimiza matakwa yake.