Surat Al-Imran, aya 27

3:27

تُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِۖ وَتُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَتُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّۖ وَتَرۡزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ ٢٧

Tūlijul-layla fin-nahāri watūlijun-nahāra fil-layli watukhrijul-hayya minal-mayyiti watukhrijul-mayyita minal-hayyi watarzuqu man tashā'u bighayri hisāb

Wewe huingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku. Na humtoa hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye hai. Na unamruzuku umtakaye bila ya hisabu. 27

Maelezo ya chini

27 Na Wewe kwa ulivyo umba na ukawekea sababu na nyendo, unauingiza usiku katika mchana kwa unavyo zidi mchana urefu wake, na unauingiza mchana katika usiku kwa unavyo zidi usiku urefu wake. Na unatoa chenye sifa za kuonekana kihai katika kisicho kuwa na sifa za uhai, kama unavyo toa chenye kukosa uhai kutokana na kilicho hai, chenye kutamakani na sababu za uhai. Unampa neema zako kubwa umtakaye kwa mujibu wa mipango ya hikima zako. Hapana mchunguzi wa kukuhisabu Wewe. Huyo Mwenye shani hii haemewi na kumjaalia Mtume wake na awapendao, ubwana, na utawala, na utajiri, na wasaa, kama alivyo waahidi.