۞ يَسۡتَبۡشِرُونَ بِنِعۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَضۡلٖ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٧١
Yastabshirūna bini'matim minallāhi wafadlin wa annallāha lā yudī'u ajral-mu'minīn
Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini. 171
Maelezo ya chini
171 Nyuso za Mashahidi zinameremeta kwa neema ya kufa shahidi na neema ya Pepo, na ubora wa karama, na ya kwamba haupotei ujira wa Waumini.