Surat Al-Imran, aya 163

3:163

هُمۡ دَرَجَٰتٌ عِندَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ ١٦٣

Hum darajātun 'indallāhi wallāhu basīru bimā ya'malūn

Hao wana vyeo mbali mbali kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote wayatendayo. 163

Maelezo ya chini

163 Makundi mawili hayo hayawi sawa, bali yametafautiana mbele ya Mwenyezi Mungu kwa daraja mbali mbali. Na Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali zao na daraja zao, na atawalipa kwa mujibu wake.