إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَلَّوۡاْ مِنكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِ إِنَّمَا ٱسۡتَزَلَّهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ بِبَعۡضِ مَا كَسَبُواْۖ وَلَقَدۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٞ ١٥٥
Innal-ladhīna tawallaw minkum yawmal-taqal-jam'āni innamastazallahumush-shaytānu biba'di mā kasabū walaqad 'afallāhu 'anhum innallāha ghafūrun halīm
Hakika wale walio rudi nyuma miongoni mwenu siku yalipo pambana majeshi mawili, Shet'ani ndiye aliye watelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyo yafanya; na Mwenyezi Mungu amekwisha wasamehe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole. 155
Maelezo ya chini
155 Enyi jamaa wa Kiislamu! Wale miongoni mwenu walio acha kusimama imara pale pahali pao walipo wekwa wasimame hakika ni Shetani ndiye aliye wavuta kwenye utelezi na kukosea kwa sababu ya makosa yao kumkhaalifu Mtume. Lakini Mwenyezi Mungu amekwisha wasamehe, kwani Yeye ni mwingi wa maghfira, na mwingi wa upole.