Surat Al-Imran, aya 145

3:145

وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِ كِتَٰبٗا مُّؤَجَّلٗاۗ وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَا وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلۡأٓخِرَةِ نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَاۚ وَسَنَجۡزِي ٱلشَّٰكِرِينَ ١٤٥

Wamā kāna linafsin an tamūta illā bi idhnillāhi kitābam mu'ajjalan waman yurid thawābad-dunyā nu'tihī minhā waman yurid thawābal-ākhirati nu'tihī minhā wasanajzish-shākirīn

Na haiwezi nafsi kuwa ife ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo andikwa ajali yake. Na mwenye kutaka malipo ya duniani tutampa; na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa. Na tutawalipa wenye kushukuru. 145

Maelezo ya chini

145 Hayumkini mtu kufa ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye amekwisha viandikia viumbe ajali yao. Na atakaye starehe ya dunia Mwenyezi Mungu atampa, na atakaye malipo ya Akhera atayapata. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao shukuru neema yake wakamt'ii kwa aliyo waamrisha ikiwa ni kupigana Jihadi au mengineyo.