زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٰتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلۡبَنِينَ وَٱلۡقَنَٰطِيرِ ٱلۡمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلۡفِضَّةِ وَٱلۡخَيۡلِ ٱلۡمُسَوَّمَةِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ وَٱلۡحَرۡثِۗ ذَٰلِكَ مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسۡنُ ٱلۡمَـَٔابِ ١٤
Zuyyina lin-nāsi hubbush-shahawāti minan-nisā'i wal-banīna wal-qanātīril-muqantarati minadh-dhahabi wal-fiddati wal-khaylil-musawwamati wal-an'āmi wal-harthi dhālika matā'ul-hayawātid-dunyā wallāhu 'indahū husnul-ma'āb
Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani; na kwa Mwenyezi Mungu ndio kwenye marejeo mema. 14
Maelezo ya chini
14 Wanaadamu wameumbwa kuwa wanapenda matamanio ya vitu kama wanawake, wana, na wingi wa madhahabu na fedha, na farasi wazuri wazuri walio fundishika, na mifugo kama ngamia, ng'ombe, mbuzi, kondoo, na kadhaalika mashamba makubwa. Lakini yote hayo ni starehe na kwa matumizi ya uhai huu wa duniani wenye kupita na kuondoka. Na hayo si chochote si lolote ukilinganisha na hisani anayo wafanyia Mwenyezi Mungu waja wake wanao pigania jihadi katika Njia yake watakapo rejea kwake Yeye Akhera.