۞ وَسَارِعُوٓاْ إِلَىٰ مَغۡفِرَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ وَجَنَّةٍ عَرۡضُهَا ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ أُعِدَّتۡ لِلۡمُتَّقِينَ ١٣٣
Wasāri'ū ilā maghfiratim mir rabbikum wajannatin 'arduhas-samāwātu wal-ardu u'iddat lil-muttaqīn
Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni Mbingu na Ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu, 133
Maelezo ya chini
133 Na kuweni wa mbele katika kutenda mema ili mpate kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye kumiliki mambo yenu yote, maghfira makubwa ya kufutiwa dhambi zenu, na Pepo yenye wasaa, na upana wake ni kama upana wa Mbingu zote na Ardhi. Hayo wametengenezewa wale wanao mcha Mwenyezi Mungu na wakaiogopa adhabu yake.