كُنتُمۡ خَيۡرَ أُمَّةٍ أُخۡرِجَتۡ لِلنَّاسِ تَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَتَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَتُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِۗ وَلَوۡ ءَامَنَ أَهۡلُ ٱلۡكِتَٰبِ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۚ مِّنۡهُمُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ ١١٠
Kuntum khayra ummatin ukhrijat lin-nāsi ta'murūna bil-ma'rūfi watanhawna 'anil-munkari watu'minūna billāhi walaw āmana ahlul-kitābi lakāna khayral lahum minhumul-mu'minūna wa aktharuhumul-fāsiqūn
Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu. 110
Maelezo ya chini
110 Nyinyi Umma wa Muhammad ni bora ya umati alio umba Mwenyezi Mungu kwa manufaa ya watu, maadamu mtaamrisha ut'iifu na mtakataza maasi, na mtakuwa ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu kwa Imani safi na ya kweli. Na lau kuwa Watu wa Kitabu wangeli kuwa ni wakweli katika imani yao kama nyinyi, basi ingeli kuwa ni bora kwao kuliko walivyo. Walakini baadhi yao ni Waumini, na wengi wao wameikiuka mipaka ya Imani na yanayo pasa.