Surat Al-Hijr, aya 51

15:51

وَنَبِّئۡهُمۡ عَن ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٥١

Wanabbi'hum 'an dayfi ibrāhīm

Na uwape khabari za wageni wa Ibrahim. 51

Maelezo ya chini

51 Ewe Nabii! Waambie pia, katika kubainisha rehema yangu makhsusi katika dunia na adhabu yangu kwa wenye kuasi humo, khabari ya Malaika walio mfikia Ibrahim kama wageni.