Surat Al-Hashr, aya 11

59:11

۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نَافَقُواْ يَقُولُونَ لِإِخۡوَٰنِهِمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَئِنۡ أُخۡرِجۡتُمۡ لَنَخۡرُجَنَّ مَعَكُمۡ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمۡ أَحَدًا أَبَدٗا وَإِن قُوتِلۡتُمۡ لَنَنصُرَنَّكُمۡ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ١١

Alam tara ilal-ladhīna nāfaqū yaqūlūna li ikhwānihimul-ladhīna kafarū min ahlil-kitābi la in ukhrijtum lanakhrujanna ma'akum walā nutī'u fīkum ahadan abadan wa in qūtiltum lanansurannakum wallāhu yashhadu innahum lakādhibūn

Huwaoni wanao fanya unaafiki wanawaambia ndugu zao walio kufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamt'ii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita lazima tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo. 11

Maelezo ya chini

11 Hebu huwaangalii hao wanaafiki ukastaajabu? Kazi yao ni kuwakariria kauli ndugu zao walio kufuru katika Watu wa Kitabu - nao ni hao Banu Nnadhir - kuwaambia: Wallahi! Mkilazimishwa kuihama Madina, basi hapana shaka na sisi tutatoka pamoja nanyi. Wala hatutamt'ii katika jambo lenu mtu yeyote daima dawamu. Na pindi ikiwa Waislamu watakupigeni vita, basi hapana shaka sisi tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hakika wanaafiki hapana shaka ni waongo katika hizo ahadi zao wanazo zitoa.