Surat Al-Hajj, aya 75

22:75

ٱللَّهُ يَصۡطَفِي مِنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ رُسُلٗا وَمِنَ ٱلنَّاسِۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعُۢ بَصِيرٞ ٧٥

Allāhu yastafī minal-malā'ikati rusulan waminan-nāsi innallāha samī'u basīr

Mwenyezi Mungu huteuwa Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona. 75

Maelezo ya chini

75 Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na hikima yake yamempelekea kuteuwa Wajumbe kutokana na Malaika, na kutokana na wanaadamu, ili wafikishe sharia yake kwa viumbe vyake. Basi huwaje mkampinga aliye mchagua Mwenyewe kuwa ni Mjumbe wake kwenu? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia wayanenayo waja wake, Mwenye kuviona vitendo wavitendavyo. Naye atawalipa kwavyo.