أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَٰبٍۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ ٧٠
Alam ta'lam annallāha ya'lamu mā fis-samā'i wal-ardi inna dhālika fī kitābin inna dhālika 'alallāhi yasīr
Je! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. 70
Maelezo ya chini
70 Ewe mwenye akili! Jua kuwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu umekusanya kila kiliomo mbinguni na duniani. Hapana kitendo cha hawa washindani kinacho fichika kwake. Vyote hivyo vimekwisha andikwa katika Ubao ulio hifadhiwa (Lauhun Mahfuudh). Kwani kujua kwake Mwenyezi Mungu na kuvithibiti kwake ni kazi nyepesi kabisa kwake.