Surat Al-Hajj, aya 66

22:66

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَحۡيَاكُمۡ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡۗ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَكَفُورٞ ٦٦

Wahuwal-ladhī ahyākum thumma yumītukum thumma yuhyīkum innal-insāna lakafūr

Na Yeye ndiye aliye kuhuisheni kisha akakufisheni, na kisha atakufufueni. Hakika mwanaadamu hana fadhila. 66

Maelezo ya chini

66 Na Yeye ndiye aliye kupeni uhai. Kisha anakufisheni unapo malizika muda wenu. Kisha tena atakufufueni Siku ya Kiyama kwa ajili ya hisabu na malipo. Hakika mwanaadamu baada ya neema zote hizi na ushahidi wote huu ni mwingi wa kumkataa Mwenyezi Mungu na kuzikataa neema zake alizo mpa.