لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ ٦٤
Llahū mā fis-samāwāti wamā fil-ardi wa innallāha lahuwal-ghaniyyul-hamīd
Ni vyake viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Mwenye kusifiwa. 64
Maelezo ya chini
64 Kila kiliomo mbinguni na katika ardhi ni chake Yeye, na kinamtumikia Yeye peke yake, na anakiendesha kama apendavyo. Na Yeye hawahitajii waja wake, bali wao ndio wanao mhitajia Yeye. Na Yeye ndiye anaye stahiki peke yake kuhimidiwa na kusifiwa na viumbe vyote.