لِّيَجۡعَلَ مَا يُلۡقِي ٱلشَّيۡطَٰنُ فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡقَاسِيَةِ قُلُوبُهُمۡۗ وَإِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ لَفِي شِقَاقِۭ بَعِيدٖ ٥٣
Lliyaj'ala mā yulqish-shaytānu fitnatal lilladhīna fī qulūbihim maradun wal-qāsiyati qulūbuhum wa innaz-zālimīna lafī shiqāqi ba'īd
Hayo ni ili alifanye lile analo litia Shet'ani liwe ni fitna kwa wale wenye maradhi ndani ya nyoyo zao, na wale ambao nyoyo zao ni ngumu. Na hakika madhaalimu wamo katika mfarakano wa mbali. 53
Maelezo ya chini
53 Na hakika Mwenyezi Mungu amewawezesha waasi wanao kataa Haki waweze kutumbukiza shakashaka na vikwazo katika Njia ya Wito ili uwe ni mtihani na majaribio kwa watu. Makafiri ambao nyoyo zao zimegeuka mawe, na wanaafiki ambao nyoyo zao zina maradhi, huzidi upotovu kwa kueneza shakashaka hizi na kuziunga mkono. Na si ajabu madhaalimu hawa kusimama msimamo huu, kwani wao wamezama katika upotovu na wamevuka mpaka katika inadi na mfarakano.