Surat Al-Hajj, aya 35

22:35

ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَٱلصَّٰبِرِينَ عَلَىٰ مَآ أَصَابَهُمۡ وَٱلۡمُقِيمِي ٱلصَّلَوٰةِ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ ٣٥

Alladhīna idhā dhukirallāhu wajilat qulūbuhum was-sābirīna 'alā mā asābahum wal-muqīmis-salawāti wamimmā razaqnāhum yunfiqūn

Ambao, anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hutetemeka, na wanao vumilia kwa yanao wasibu, na wanao shika Swala, na wanatoa katika tulivyo waruzuku. 35

Maelezo ya chini

35 Wale ambao akitajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hupapatika kwa kumkhofu, na hunyenyekea kwa kutajwa kwake, na ambao wanasubiri kwa masaibu ya karaha na shida yanayo wapata kwa kujisalimisha mbele ya amri yake na hukumu yake, na wakashika Swala kwa ukamilifu wake, na wakatoa baadhi ya mali aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu katika njia za kheri.