Surat Al-Hajj, aya 32

22:32

ذَٰلِكَۖ وَمَن يُعَظِّمۡ شَعَٰٓئِرَ ٱللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقۡوَى ٱلۡقُلُوبِ ٣٢

Dhālika waman yu'azzim sha'ā'irallāhi fa innahā min taqwal-qulūb

Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo. 32

Maelezo ya chini

32 Hakika mwenye kuitukuza Dini ya Mwenyezi Mungu na faridha ya Hija na a'mali zake na mihanga inayo pelekwa kwa ajili mafakiri wa Al-Haram, na wakachagua walio nona wazima, hawana ila, basi huyo ndio amemcha Mwenyezi Mungu. Kwani kutukuza kwake hayo ni matokeo ya unyenyekevu wa nyoyo zilizo amini, na alama katika alama za usafi wa niya.