Surat Al-Furqan, aya 10

25:10

تَبَارَكَ ٱلَّذِيٓ إِن شَآءَ جَعَلَ لَكَ خَيۡرٗا مِّن ذَٰلِكَ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ وَيَجۡعَل لَّكَ قُصُورَۢا ١٠

Tabārakal-ladhī in shā'a ja'ala laka khayram min dhālika jannātin tajrī min tahtihal-anhāru wayaj'al laka qusūrā

Ametukuka ambaye akitaka atakujaalia yaliyo bora kuliko hayo,nayo ni mabustani yapitayo mito kati yao, na atakujaalia majumba ya fakhari. 10

Maelezo ya chini

10 Mwenyezi Mungu ametukuka, na izidi kheri yake! Yeye ndiye ambaye pindi akitaka atakujaalia duniani bora kuliko hayo wanayo pendekeza wao. Kwa Akhera Yeye amekwisha kujaalia kama alivyo kuahidi, nayo ni mabustani mengi yapitayo mito pembezoni mwake, na baina ya miti yake, na majumba ya fakhari madhubuti.