Surat Al-Bayyinah, aya 5

98:5

وَمَآ أُمِرُوٓاْ إِلَّا لِيَعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ حُنَفَآءَ وَيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ ٱلۡقَيِّمَةِ ٥

Wamā umirū illā liya'budullāha mukhlisīna lahud-dīna hunafā'a wayuqīmus-salawāta wayu'tuz-zakawāta wadhālika dīnul-qayyimah

Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti. 5

Maelezo ya chini

5 Na hawakulazimishwa jambo katika walio lazimishwa ila iwe ibada yao kwa Mwenyezi Mungu ni kumsafia Yeye Dini, waache upotovu wasimame sawa kwenye Haki, na wazihifadhi Swala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Mila Iliyo Nyooka.