Surat Al-Baqarah, aya 91

2:91

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ ءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ نُؤۡمِنُ بِمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَيَكۡفُرُونَ بِمَا وَرَآءَهُۥ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَهُمۡۗ قُلۡ فَلِمَ تَقۡتُلُونَ أَنۢبِيَآءَ ٱللَّهِ مِن قَبۡلُ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ٩١

Wa idhā qīla lahum āminū bimā anzalallāhu qālū nu'minu bimā unzila 'alaynā wayakfurūna bimā warā'ahū wahuwal-haqqu musaddiqal limā ma'ahum qul falima taqtulūna ambiyā'allāhi min qablu in kuntum mu'minīn

Na wanapo ambiwa: Yaaminini aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu. Wao husema: Tunaamini tuliyo teremshiwa sisi. Na huyakataa yasiyo kuwa hayo. Na hali ya kuwa hii ndiyo Haki inayo thibitisha yale waliyo nayo wao. Sema: Mbona mliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu hapo zamani ikiwa kweli mlikuwa Waumini? 91

Maelezo ya chini

91 Hizi ndizo dhamiri walizo nazo ndani ya nafsi zao. Lakini mbele za watu wakijitetea kuwa wao hawaiamini Qur'ani wanapo takiwa waamini, kwa kuwa wao hawaamini ila yale walio teremshiwa wao tu, na wanayakataa mengineyo. Na hakika wanasema uwongo kwa hayo madai yao kuwa wanaamini yaliyomo katika Taurati, kwani kwa kukitaa Kitabu hichi cha Qur'ani kinacho thibitisha Kitabu chao, ndio kuwa maana yake wanakataa Kitabu chao chenyewe, na kwa kuwa wao waliwauwa Manabii walio kuwa wanawaitia yale walio teremshiwa. Na wao kuwauwa hao ni dalili ya kukata kuwa hawauamini Ujumbe wao.