Surat Al-Baqarah, aya 55

2:55

وَإِذۡ قُلۡتُمۡ يَٰمُوسَىٰ لَن نُّؤۡمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى ٱللَّهَ جَهۡرَةٗ فَأَخَذَتۡكُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ ٥٥

Wa idh qultum yāmūsā lan nu'mina laka hattā narallāha jahratan fa akhadhatkumus-sā'iqatu wa antum tanzurūn

Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi. Ikakunyakueni radi nanyi mnaangalia. 55

Maelezo ya chini

55 Na kumbukeni kauli yenu mlio mwambia Musa: Kwamba sisi hatukukubali wewe mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi hivi hivi kwa macho bila ya kificho. Ikakuchukueni radi na moto kutoka mbinguni, ikakutikiseni kuwa ni malipo ya inadi yenu na dhulma zenu, na kutaka kwenu jambo ambalo ni muhali kutokea kwenu. Nanyi mnaiona hali yenu na balaa na adhabu zilizo kusibuni kwa mpigo wa radi hiyo.