Surat Al-Baqarah, aya 42

2:42

وَلَا تَلۡبِسُواْ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُواْ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ٤٢

Walā talbisul-haqqa bil-bātili wataktumul-haqqa wa antum ta'lamūn

Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua. 42

Maelezo ya chini

42 Wala msichanganye Haki iliyo toka kwangu na upotovu mlio uzua nyinyi, hata ikawa halijuulikani la kweli na la uwongo. Wala msiifiche Haki, na katika hiyo Haki ni kumsadiki Muhammad, na nyinyi mnajua kuwa yeye ni wa kweli na wa kusadikiwa.