قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ لَا عِلۡمَ لَنَآ إِلَّا مَا عَلَّمۡتَنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ ٣٢
Qālū subhānaka lā 'ilma lanā illā mā 'allamtanā innaka antal-'alīmul-hakīm
Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima. 32
Maelezo ya chini
32 Malaika wakatambua upungufu wao, wakasema: Sisi tunakutakasa Ewe Mola wetu Mlezi kwa mtakaso ulio laiki nawe. Tunakiri kuwa tumeshindwa, na hatuwezi kupinga. Kwani hatuna ilimu kuliko uliyotupa Wewe, na Wewe ndiye Mjuzi wa kila kitu, na Mwenye hikima na hukumu katika kila jambo ulitendalo.