Surat Al-Baqarah, aya 277

2:277

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ٢٧٧

Innal-ladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti wa aqāmus-salawāta wa ātawuz-zakawāta lahum ajruhum 'inda rabbihim walā khawfun 'alayhim walā hum yahzanūn

Hakika wale walio amini na wakatenda mema na wakashika Swala na wakatoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. 277

Maelezo ya chini

277 Hakika wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na wakazitimiza amri zake, na wakatenda mema aliyo waamrisha, na wakaacha yaliyo katazwa ya haramu, na wakatimiza Swala kwa njia ya ukamilifu, na wakatoa Zaka kuwapa wanao stahiki, watapata thawabu kubwa mno walio wekewa kwa Mola wao. Na wala hawatakuwa na khofu ya chochote kwa siku zijazo, wala hawatahuzunika kwa lolote walilo likosa.