يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنفِقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا بَيۡعٞ فِيهِ وَلَا خُلَّةٞ وَلَا شَفَٰعَةٞۗ وَٱلۡكَٰفِرُونَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ ٢٥٤
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū anfiqū mimmā razaqnākum min qabli an ya'tiya yawmul lā bay'un fīhi walā khullatun walā shafā'atun wal-kāfirūna humuz-zālimūn
Enyi mlio amini! Toeni katika tulivyo kupeni kabla haijafika Siku ambayo hapatakuwapo biashara, wala urafiki, wala uombezi. Na makafiri ndio madhaalimu. 254
Maelezo ya chini
254 Enyi mlio muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho! Toeni baadhi ya tuliyo kuruzukuni kwa ajili ya mambo ya kheri. Fanyeni haraka kwa hayo kabla haijafika Siku ya Kiyama ambayo itayo kuwa yote ni ya kheri, wala hazipatikani sababu za kuzozana. Siku hiyo hamwezi kuyadiriki yaliyo kwisha kupiteni duniani, na hapo haitakufaeni biashara, wala urafiki, wala uombezi wa mtu yeyote bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu. Na siku hiyo dhulma za makafiri zitadhihiri kwa kuwa hawakuitikia Wito wa Haki.