Surat Al-Baqarah, aya 230

2:230

فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُۥ مِنۢ بَعۡدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوۡجًا غَيۡرَهُۥۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَآ أَن يَتَرَاجَعَآ إِن ظَنَّآ أَن يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِۗ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ ٢٣٠

Fa in tallaqahā falā tahillu lahū mim ba'du hattā tankiha zawjan ghayrahū fa in tallaqahā falā junāha 'alayhimā an yatarāja'ā in zannā an yuqīmā hudūdallāhi watilka hudūdullāhi yubayyinuhā liqawmin ya'lamūn

Na kama amempa t'alaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayo ibainisha kwa watu wanao jua. 230

Maelezo ya chini

230 Mume akimwacha mkewe mara ya tatu baada ya T'alaka mbili za mwanzo basi hamhalalikii mpaka yule mke aolewe na mume mwengine aingie harusi. Akimwacha baada ya hapo basi anaweza kufunga ndoa tena na yule mume wa kwanza, na wala hapana dhambi juu yao kuanza maisha mapya kwa ndoa mpya. Lakini yawapasa waazimie kuendesha maisha mema ya mume na mke wakifuata sharia alizo ziwekea mipaka Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la. Na mipaka hii imebainishwa wazi kwa mwenye kuamini sharia ya Kiislamu na anataka ilimu na a'mali njema.