نِسَآؤُكُمۡ حَرۡثٞ لَّكُمۡ فَأۡتُواْ حَرۡثَكُمۡ أَنَّىٰ شِئۡتُمۡۖ وَقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُم مُّلَٰقُوهُۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٢٢٣
Nisā'ukum harthul lakum fa tū harthakum annā shi'tum waqaddimū li anfusikum wattaqullāha wa'lamū annakum mulāqūhu wabasshiril-mu'minīn
Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana naye. Na wape bishara njema Waumini. 223
Maelezo ya chini
223 Wake zenu ni mwahali mwa kupatia uzazi, kama vile mbegu inavyo toa mmea. Basi ni halali kwenu kuwaingilia vyovyote kwa sharti ya kupitia njia za uzazi. Na mcheni Mwenyezi Mungu wala msimuasi katika kukaa kwenu na wanawake. Na mjue kuwa nyinyi mtakutana naye, na mna jukumu kwake. Furaha ni ya hao wanao simama juu ya mipaka yake Mtukufu na hawaikiuki.