Surat Al-Baqarah, aya 215

2:215

يَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَۖ قُلۡ مَآ أَنفَقۡتُم مِّنۡ خَيۡرٖ فَلِلۡوَٰلِدَيۡنِ وَٱلۡأَقۡرَبِينَ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِۗ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ ٢١٥

Yas'alūnaka mādhā yunfiqūna qul mā anfaqtum min khayrin falil-wālidayni wal-aqrabīna wal-yatāmā wal-masākīni wabnis-sabīli wamā taf'alū min khayrin fa innallāha bihī 'alīm

Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. 215

Maelezo ya chini

215 Waumini wanakuuliza mas-ala ya kutoa. Waambie: Kutoa iwe kutokana na mali mazuri, na wa kupewa ni wazazi wawili, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri aliye katikiwa na mali yake na watu wake. Na lolote katika vitendo vya kheri mlitendalo basi hakika Mwnyezi Mungu analijua na atakulipeni kwalo.