Surat Al-Baqarah, aya 2

2:2

ذَٰلِكَ ٱلۡكِتَٰبُ لَا رَيۡبَۛ فِيهِۛ هُدٗى لِّلۡمُتَّقِينَ ٢

Dhālikal-kitābu lā rayba fīhi hudal lil-muttaqīn

Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu, 2

Maelezo ya chini

2 Hichi ndicho Kitabu kilicho kamilika, kisicho kuwa na dowa, nacho ni Qur'ani tunayo iteremsha isiyo tiliwa shaka yoyote na kila mwenye akili na mwenye insafu akajua kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Wala haitilii shaka kuwa yasemwayo juu ya mambo na hukumu ni ya kweli tupu. Ndani ya Kitabu hichi upo uwongofu ulio kamilika kwa walio kuwa tayari kuitafuta Kweli, na wanajikinga na madhara na mambo ya kuwaletea adhabu.