ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِي ٱلۡكِتَٰبِ لَفِي شِقَاقِۭ بَعِيدٖ ١٧٦
Dhālika bi annallāha nazzalal-kitāba bil-haqqi wa innal-ladhīnakhtalafū fil-kitābi lafī shiqāqi ba'īd
Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki. Na wale walio khitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani ulio mbali na haki. 176
Maelezo ya chini
176 Nao yamewapasa malipo waliyo kadiriwa kwa kukikataa Kitabu cha Mwenyezi Mungu alicho kiteremsha kwa haki na kweli. Na wamekhitalifiana kwacho khitilafu kubwa iliyo wapelekea kupenda kujadiliana na kujitenga na Haki, na kufuata pumbao, wakakigeuza na kukifisidi na kukifasiri kinyume na maana yake ya hakika.