ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ ١٤٧
Al-haqqu mir rabbika falā takūnanna minal-mumtarīn
Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka. 147
Maelezo ya chini
147 Na hakika Haki ni anayo kutolea Mwenyezi Mungu Mtukufu sio wanayo kupotoshelea watu wa Kitabu. Basi kuweni na yakini nayo, msiwe watu wenye kutia shaka shaka na kubabaika. Na katika hiyo Haki ni hii amri ya Kibla, basi endeleeni nayo wala msiwabali (musiwajali) wapinzani.