تِلۡكَ أُمَّةٞ قَدۡ خَلَتۡۖ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَلَكُم مَّا كَسَبۡتُمۡۖ وَلَا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ١٤١
Tilka ummatun qad khalat lahā mā kasabat walakum mā kasabtum walā tus'alūna 'ammā kānū ya'malūn
Hao ni watu walio kwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na nyinyi mtapata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa wakifanya wao. 141
Maelezo ya chini
141 Tena imekuwaje nyinyi Mayahudi na Wakristo kuyajadili mambo ya watu hawa? Kwani watu hawa wamekwisha pita na njia zao. Wao watapata malipo ya a'mali yao waliyo itenda katika uhai wao, wala nyinyi hamtaulizwa juu ya a'mali zao, wala hamtafaidika kwa lolote katika hayo. Nanyi hamtapata malipo ila kwa vitendo mnavyo vifanya nyinyi wenyewe.