وَلَن تَرۡضَىٰ عَنكَ ٱلۡيَهُودُ وَلَا ٱلنَّصَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمۡۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۗ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ ٱلَّذِي جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ ١٢٠
Walan tardā 'ankal-yahūdu walan-nasārā hattā tattabi'a millatahum qul inna hudallāhi huwal-hudā wala'init-taba'ta ahwā'ahum ba'dal-ladhī jā'aka minal-'ilmi mā laka minallāhi min waliyyin walā nasīr
Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu. 120
Maelezo ya chini
120 Basi usijikere nafsi yako kwa kutaka kuwaridhi hao wapinzani wa Kiyahudi na Wakristo. Kwani hao hawatakuwa radhi nawe mpaka ufuate mila yao hao ambao wanadai ati ndio wenye uwongofu. Na kabisa hapana uwongofu ila uwongofu wa Mwenyezi Mungu ulioko katika Uislamu. Na mwenye kufuata matamanio ya watu hawa baada ya kuijua Haki tuliyo kuteremshia wewe, basi Siku ya Kiyama hatapata mlinzi wa kumsaidia mbele ya Mwenyezi Mungu, wala hatapata wa kumnusuru na adhabu.