وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ١١٠
Wa aqīmus-salawāta wa ātuz-zakawāta wamā tuqaddimū li anfusikum min khayrin tajidūhu 'indallāhi innallāha bimā ta'malūna basīr
Na shikeni Swala na toeni Zaka; na kheri mtakazo jitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yafanya. 110
Maelezo ya chini
110 Na hifadhini mambo ya Dini yenu: Shikeni Swala, toeni Zaka, na vitendo vyote vyema mnavyo fanya kujitangulizia nafsi zenu, na sadaka mnazo toa, malipo yake mtayakuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua vyema myatendayo; ujuzi wake ni ujuzi wa mwenye kutazama akaona.