ثُمَّ بَدَّلۡنَا مَكَانَ ٱلسَّيِّئَةِ ٱلۡحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَواْ وَّقَالُواْ قَدۡ مَسَّ ءَابَآءَنَا ٱلضَّرَّآءُ وَٱلسَّرَّآءُ فَأَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ٩٥
Thumma baddalnā makānas-sayyi'atil-hasanata hattā 'afaw wwaqālū qad massa ābā'anad-darrā'u was-sarrā'u fa akhadhnāhum baghtatan wahum lā yash'urūn
Kisha Sisi hubadilisha mahala pa ubaya kwa wema, hata wakazidi, na wakasema: Taabu na raha ziliwafikia baba zetu. Basi kwa ghafla tukawashika, hali ya kuwa hawajatambua. 95
Maelezo ya chini
95 Basi tena ilivyo kuwa hawakufanya hayo, bali wakaendelea na ukafiri wao na inadi yao, tukawapa mtihani wa kuwapa neema badala ya dhiki ili kuwapururia tu. Tukawapa kutononoka, na nafasi nzuri, na siha na afya, mpaka wakawa wengi, na mali yao yakazidi, wakasema kwa ujinga wao: Hayo yaliyo wapata baba zetu ya mahna, na balaa, na starehe na neema - hayo yote ndio shani ya ulimwengu. Shida na neema huwajia watu kwa zamu. Hawakuzindukana wakajua kuwa haya ni malipo ya kufru zao wakajizuia! Na kwa hivyo wakawa hawaujui mwendo wa Mwenyezi Mungu, iliyo tukuka shani yake, katika sababu za matengenezo na uharibifu wa binaadamu, na nini linalo leta neema na nini linalo leta dhiki! Matokeo ya hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu aliwapatiliza kwa kuwaletea adhabu ya kuteketeza kwa ghafla, na wao bila ya kujua nini litawafika.