Surat Al-A'raf, aya 86

7:86

وَلَا تَقۡعُدُواْ بِكُلِّ صِرَٰطٖ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ بِهِۦ وَتَبۡغُونَهَا عِوَجٗاۚ وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ كُنتُمۡ قَلِيلٗا فَكَثَّرَكُمۡۖ وَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ ٨٦

Walā taq'udū bikulli sirātin tū'idūna watasuddūna 'an sabīlillāhi man āmana bihī watabghūnahā 'iwajan wadhkurū idh kuntum qalīlan fakattharakum wanzurū kayfa kāna 'āqibatul-mufsidīn

Wala msikae katika kila njia mkitisha watu, na kuwazuilia na Njia ya Mwenyezi Mungu wale wenye kumuamini, na mkataka njia ipotoke. Na kumbukeni mlipo kuwa wachache, naye akakufanyeni kuwa wengi. Na tazameni jinsi ulivyo kuwa mwisho wa mafisadi. 86

Maelezo ya chini

86 Wala msikae katika kupinga kila njia za Haki na uwongofu na a'mali njema, mkiwatishia wapitao, na kwa hivyo mkawazuia watafutao kheri wasiifikie. Nao hao ndio watu wa Imani wanao muamini Mwenyezi Mungu, nanyi mnaitaka njia iliyo potoka! Na kumbukeni mlivyo kuwa ni watu wachache, Mwenyezi Mungu akakufanyeni mkawa wengi kwa kwenda sawa kutaka uzazi na mali. Na zingatieni nini ulikuwa mwisho wa waharibifu walio kuwa kabla yenu.