وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ جَعَلَكُمۡ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعۡدِ عَادٖ وَبَوَّأَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورٗا وَتَنۡحِتُونَ ٱلۡجِبَالَ بُيُوتٗاۖ فَٱذۡكُرُوٓاْ ءَالَآءَ ٱللَّهِ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ ٧٤
Wadhkurū idh ja'alakum khulafā'a mim ba'di 'ādin wabawwa'akum fil-ardi tattakhidhūna min suhūlihā qusūran watanhitūnal-jibāla buyūtan fadhkurū ālā'allāhi walā ta'thaw fil-ardi mufsidīn
Na kumbukeni alivyo kufanyeni wa kushika pahala pa A'adi na akakuwekeni vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msitende uovu katika nchi kwa ufisadi. 74
Maelezo ya chini
74 Na kumbukeni kuwa Mwenyezi Mungu amekujaalieni ndio wa kurithi nchi ya A'ad, na akakupeni katika hiyo nchi makaazi mema, mkijenga majumba ya fakhari katika nyanda zake. Na mkichonga milima mkifanya majumba. Basi kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, alivyo kuwekeni kwa makini katika nchi, wala msifanye maovu katika nchi, mkawa wenye kufisidi na kuharibu baada ya kukaa kwa makini kama huku.